No internet connection


Wishlist

Kuhusu

 Ndugu mtumiaji wa App hii ya tiba asili na Jadi, 

Tunapenda kukufahamisha kuwa Lengo kubwa la App hii ni kukuwezesha kujifunza mambo mablimbali yanayohusu tiba za jadi ambayo ndio asili yetu Waafrika.

App hii au vitabu utavyovipata hapa havilengi kukufundisha au kukushawishi kufanya mambo yasiyofaa kama vile uchawi n.k.

Hatutokuwa ni wenye kuwajibika kwa mujibu wa sheria ikiwa utadhurika kwa namna yoyote ile kwa kujaribu kufata kwa vitendo yale yaliyoandikwa hapa bila kupata maelekezo ya zaidi kutoka kwa mtaalam, Ingawa dawa zote za tibajadi zilizo orodheshwa  hapa ni salama kwa matumizi na kwa kutibu ugonjwa ulioainishwa.

Maudhui haya ni salama kwa wewe kujifunza mimea mbalimbali na kazi zake, kujifunza elimu ya viumbe na kukupa uelewa juu ya mambo yanayofanywa na wachawi ili kuweza kujikinga nayo.

App hii ni maalumu kwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 35+, ikiwa una umri chini ya miaka hiyo unashauriwa kufuta App katika simu yako.

Kumbuka App hii ni bure kabisa, michango unayochangia haisimami kama malipo ya kutumia App bali ni mchango kwa ajili ya kuendeshea App hii na kuifanya iendelee kuwepo. Hivyo utachangia tu ikiwa umeguswa na maudhui ya App na si vinginevyo. 

Kwa maswali, msaada juu ya yale yaliyoandikwa humu au hayapo unaweza kutuuliza kupitia kitufe cha msaada .

App hii haikusanyi taarifa binafsi kama vile jina la mtumiaji, umri na jinsia. Tunaweza kukusanya namba ya simu ikiwa utachangia mchango wako au kuhitaji kuwasiliana nasi. Namba yako haitotumika kinyume na lengo lililowasilishwa. Ikiwa hauhitaji tena namba yako kuendelea kuhifadhiwa nasi, unaweza kuwasiliana nasi kuruhusu kufutwa kwa namba yako.


arrow_back

bookmark visibility